Saturday, August 12, 2017

DIWANI WA KATA SAMBASHA ( CCM) AACHIWA KWA DHAMANA DHIDI YA KESI INAYOMKABILI

Na Vero Ignatus.Arusha

Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imemsomea mashtaka mawili aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini .

Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo kosa la kwanza alituhumiwa kujifanya Afisa mtumishi wa serekali (TISS)huku kosa la pili ikiwa kugushi moja ya nyaraka za serekali(kitambulisho ).

Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo Wakili wa serekali Penina Joakim amesema kuwa Mnamo May 18 katika hotel ya Skyway iliopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa alijitambulisha kama Afisa utumishi wa idara ya usalama wa taifa na kufanya Utapeli .

Wakili Penina alitaja kosa la pili ambalo Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka jamuhuri ya muungano wa Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi maalumu Agent (undercover)chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni kinyume cha kisheria .

Hata hivyo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka ndipo Hakimu Mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Nestory Barro alisema dhamana ipo wazi iwapo wathamini watakithi vigezo vinavyotakiwa na mahakama hiyo.

Hata hivyo Mshitakiwa alipata dhamana baada ya kukithi vigezo vilivyowekwa na mahakama ambapo ilikuwa ni wadhamini wawili wenye sifa ambapo kwanza awe mtumishi wa serikali pili awe na mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa kila mmoja.

Hata hivyo wakili Edina Mndeme anayemtetea Lengai Ole Sabaya amesema kuwa mteja wake amekuwa akifikishwa mahakamani na amesomewa mashitaka yaleyale na hii ni mara ya nne .

Kesi imeaihishwa na hakimu mkazi hadi itakapotajwa tena 30/8/2017 ambapo uchunguzi unatarajiwa kukamilika na kesi hiyo kuanza kusikilizwa.
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akiwa nje ya mahakama mara baada ya kuachiwa kwa dhamana kutokana na kesi inayomkabili.Picha na Vero Ignatus Blog.
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akizungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama.Picha na Vero Ignatus Blog.
Akizungumza na mwenyekiti wa CCM katika kata ya Sambasha Lesion Letionoki Njoki.Picha na Vero Ignatus Blog.

Akisalimiana na wananchi wa kata ya Sambasha mara baada ya kuachiwa kwa dhamana.Picha na Vero Ignatus Blog.

No comments: