Wednesday, May 31, 2017

KAMPUNI YA ALLIANCE ONE YAANDAA UTARATIBU WA KUPANDA MITI KWA KILA MSIMU WA KILIMO WILAYANI KASULU.

TUMBAKU ni zao ambalo husababisha uharibifu wa Misitu katika uzalishaji wa tumbaku ya Mvuke, kwa kukabiliana na Changamoto hiyo Kampuni ya kuuza na Kununua tumbaku ya Alliance one Wilayani Kasulu imeandaa utaratibu wa kupanda Miti kwa kuwashirikisha Wakulima kutoa Ardhi yao na halmashauri kwa kupanda hekta 288 kwa kila msimu wa kilimo lengo ikiwa ni kuhakikisha kuni zinazotumika katika uchomaji wa tumbaku zinatoka katika chanzo endelevu cha miti wanayoipanda. 

Akizungumza mara baada ya makabidhiano ya Mashamba ya Miti hekta 144 jana yalitooteshwa kwa kipindi cha mwaka 2014 - 2015 katika Kijiji cha Mganza na Chogo kata ya Heru juu baina ya halmashauri na kampuni hiyo Meneja uzalishaji jani katika Kampuni hiyo, David Mayunga, alisema kampuni hiyo inajihusisha na uendelezaji wa nishati mbadara ya kuchomea tumbaku, kuborsha mabani ya kuchomea iliyaweze kutumia kuni chache.

Mayunga alisema uzalishaji wa tumbaku ya Mvuke unategemea kiasi kikubwa cha kuni hapa Tanzania na Nchi nyingine pia na husababisha uteketezaji wa misitu, kampuni hiyo wamedhamilia kuwa ifikapo mwaka 2020 uzalishaji wa tumbaku utatumia kuni kutoka katika vyanzo endelevu ambapo Wakulima na serikali watatoa maeneo yao waweze kupandiwa miti lengo ikiwa ni kuinua uzalishaji wa tumbaku pamoja na Wakulima.

Alisema tumbaku ni zao la pili kwa Tanzania linalo ingiza fedha za kigeni, kampuni hiyo inafanya zoezi hilo katika maeneo ambayo yanalima tumbaku ilikuweza kiwasaidia Wakulima kutunza mazingira na kufanya biashara ya tumbaku bila kiathiri mazingira, kwa kipindi kilicho pita zao la tumbaku limeshuka sana kutokana na Wakulima wengi kushindwa kulima kutokana na gharama ya zao hilo.

"Pamoja na malengo tuliyonayo ya kuinua zoezi la upandaji miti tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Ardhi hili linatokana na baadhi ya Wananchi kuzuia mashamba yao yasipandwe miti kwa kuhofia kwamba watazulumiwa, kukosekana kwa ushirikiano baina ya Viongonzi na kampuni hili linasababisha kampuni kushindwa kupanda miti kwa malengo yaliyo pangwa", alisema Mayunga.

Alisema zoezi hilo kwa misimu ilyopita walifanikiwa kwa asilimia 85% na siku ya jana walikabidhi kiasi cha hekta 68.7 kwa kijiji cha Chogo na hekta 76.4 zitakabidhiwa Kwa wananchi walioyoa mashamba yao katika kijiji cha Mganza, hata hivyo aliwaomba Wananchi kuendelea kujitolea mashamba yao waweze kupandiwa miti hiyo kwakuwa faida ya miti hiyo wataipata wao na sio kampuni na gharama zote za upandaji na usimamizi zitafanywa na Kampuni.

Kwa upande wake Katibu tawala wa Wilaya ya Kasulu Titus Mguha aliishukuru kwampuni hiyo kwaniaba ya serikali kwa hatua ya kuanza kupanda miti katika Vijiji hivyo hatua hiyo itasaidia kuboresha mazingira na kurudisha misitu kwa maeneo ambayo yalikuwa yameharibiwa na Wakulima na wafugaji na kwasasa watatumia misitu yao binafsi.

Alisema Wananchi wanatakiwa kutoa ardhi kwa Kampuni hiyo kwakua kampuni hiyo inalengo zuri la kuhakikisha Wakulima Watumbaku hawaangaiki kutumia misitu ya asili na badala yake watatumia miyi ambayo wanaipanda katika Misitu hao na kuweza kufanya kilimo cha tumbaku bila kuathiri misitu ya asili.

Nae Mwenyekiti Wa halmashauri ya Mji wa Kasulu , Twallib Mangu alisema Wao kama halmashauri watajitahidi kuingiza suala hilo la upandaji miti katika vikao vyao na Madiwani waweze kuwahamasisha Wananchi wao kitoa ardhi zao kwaajili ya kupandiwa miti ilikuhakikisha na wao wananufaika na mradi huo na kuweza kupata mafanikio ya uhifadhi wa misitu.

Aidha aliiiomba kampuni hiyo kuandaa mikataba itakayo waonyesha ni jinsi  gani Mwananchi atanufaika na mradi huo na kampuni itanufaika na nini ilikuwaondoa Wananchi wasiwasi wa kuhofia kuibiwa , na aliwaomba Wananchi kuwatumia Wanansheria wa Halmashauri kabla ya kusainishwa mikataba hiyo na kuweza kujitokeza kwa wingi waweze kupandiwa miti hiyo.

Baadhi ya Wananchi Lisa Ramadhani na Hatibu Juma waliipongeza sana kampuni hiyo na kuishukuru kwa kuwapandia moti na kwamba miti huiyo itawasaidia kupata kuni na kupata mbao za kujengea na manufaa mengi hivyo wakotayari kujitolea mashamba yao iliwaweze kupandiwa miti hiyo.

Wenceraus Mbuyeko alisema yeye kwa upande wake atatoa hekari 16 waweze kumpandia miti katika shamba lake kwakuwa faida anaziona na baadhi ya Wananchi waliopandiwa miti wanaendelea kunufaika na miti hiyo, kampuni hiyo inamipango mizuri ya kuweza kuinua kilimo cha wakulima wa tumbaku.
 Meneja wa uzalishaji jani wa kampuni ya Alliance one David Mayunga  akisain hati ya makabidhiano ya mashamba ya  miti kwa Halmashauri ya Wilaya ya kasulu.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa kasulu Twallib Mangu, akisaini baadhi ya mikataba ya makabidhiano baina ya kampuni ya Alliance one na halmashauri.

No comments: