Sunday, June 30, 2013

SPERANSIA MHONDELE NI BINTI WA MIAKA 18 MWENYE NDOTO LA KULITANGAZA TAIFA KISOKA

Mwanadada  mkali  wa soka  Iringa na mikoa ya nyanda za juu  kusini Speransia Mhondele  akionyesha uwezo wake  kisoka
Hapa  aklionyesha jinsi ya  kutuliza mpira  kwa gamba
Akionyesha mbinu ya  kumkabili  adui  kwa mpira  wa angani
Hapa  akijiandaa kuondoka na mpira  baada ya  kuutuliza  kutoka hewani


Timu ya  watuma  salam mkoa wa Iringa ambayo  binti Speransia ( wa pili  kushoto waliosimama) alipata  kuonyesha soka la uhakika  jana wakati wa mchezo wa kirafikin kati ya  watangazaji wa radio  Furaha Fm na  watuma  salam mchezo uliomalizika kwa  watangazaji  kushinda  baada ya kuigagadua timu ya  watuma  salam mabao 2-0
.......................................................................................

Spransia  Evaristo Mhondele ni  binti  wa miaka 18  mkazi  wa Kihesa katika manispaa ya Iringa mwenye  kipaji  cha hali ya  juu katika mchezo  wa mpira  wa  miguu mwenye ndoto  za kuj kulipa heshima  kubwa Taifa la Tanzania  katika soka la  wanawake .

“mimi nilihitimu masomo yangu ya  sekondari mwaka 2012 katika  shule ya  sekondari Mlamke katika Manispaa ya  Iringa na  nimepata  kuchaguliwa kujiunga na timu  za UMISETA katika mchezo wa  soka wanawake “

Nilianza  kucheza mpira  mwaka mwaka 2010 nikiwa katika mashindano ya UMISETA  yaliyofanyika katika Ifunda kwa wilaya ya  Iringa  ambako nilikwenda  kushiriki mchezo  wa Basketi  .

Baada ya  kufika  huku nilikuta kuna ushindani mkubwa katika mchezo huo ambao  nilichaguliwa na  hivyo baada ya   kuchujwa  wengi nikiwemo mimi katika mchezo huo  ndipo  nillipoamua  kubadili mchezo na  kuanza kucheza mchezo wa mpira wa  miguu kwa  kufanya mazoezi .

Nilifanya mazoezi  usiku na mchana na baada ya mashindano mengine ya  UMISETA ndipo nilipoamua  kuelekeza  nguvu  huko na kujiunga kabisa katika timu ya mpira wa miguu ya  wanawake .

Kujiunga kwangu na  timu ya  mpira  wa  miguu wanawake  kuniliwezesha  kupita hatua kwa  kuchaguliwa  kuwakilisha  mkoa  wa Iringa katika mashindano ya kanda ya  kusini  kwa  kuelekea  mkoani Ruvuma kwa mara  ya kwanza kufika katika mkoa  huo na baada ya kufanya vizuri huko  nilichaguliwa  kuwakilisha kanda  ya kusini katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani .

“ Jitihada  binafsi nilizoonyesha  na  wachezaji wenzangu  tuliiwezesha  timu  yetu  kutoka  kanda ya nyanda za juu kusini  kushika nafasi ya  tatu kitaifa “

Mchezaji  huyo anadai kuwa  ndoto yake  kubwa katika soka  kuja kuchezea timu  kubwa  za  kitaifa ili   kuweza  kuonyesha uwezo  wake  zaidi .

“Kwa  sasa  nasuburi  ruhusa ya  mzazi  wangu  ili  kuweza  kuniruhusu   kujikita  zaidi katika michezo  ili  kuweza  kutafuta  fursa ya  kulitumikia  Taifa  langu  Tanzania katika michezo …..nilishindwa  kujiunga na  timu  za  wanawake  nje ya mkoa  kutokana na  wazazi  kunizuia kutokana na  wakati huo  nilikuwa masomoni “

Spransia  anasema  kuwa  katika maisha  yake wakati akiwa  shule  kwa sehemu  kubwa alikuwa akiwaza  michezo zaidi  na  hasa  kuwa na ndoto ya  kuja  kuchezea timu kubwa za  mpira  wa miguu kwa  wanawake na yawezekana  hata kufeli kwake  kulitokana na mawazo ya  michezo .

Hata  hivyo anasema  kuwa kati ya mambo ambayo katika maisha  anaona  bado  kufanikiwa na hana ndoto ya  kukimbilia  kuolewa  wala katika  mahusiano na  wanaume kwa sasa ni kutokana na  kutotimiza  azma yake ya  kuchezea  timu  kubwa ya  soka  wanawake  nje ya  mkoa  wa Iringa .

Kwani amesema katika mashindano ya  UMISETA kwa jitihada  zake binafsi amepata  kuifungia  timu yake magoli matatu na  kuwa kwa  sasa baada ya  kuhitimu  elimu ya  sekondari amepata kuchezea  timu mbali mbali kama  Kwa kilosa FC , Sengo FC na  timu  ya  watuma  salam mkoa  wa Iringa  wanaume ambapo kwa upande upande wa  Sengo Fc nimepata  kufunga magoli mawili .

Pia  amesema  kuwa anaomba  chama  cha mpira  wa miguu  wanawake  Taifa  iwapo  kuna  nafasi ya  kusajili  wachezaji  wapya  kuweza  kumtazama hata  kumpa nafasi ya majaribio  ili aweze  kuonyesha kipaji chake .

Mwandishi  wa makala  haya  alipata  kushuhudia kandanda safi iliyoonyeshwa na mchezaji  huyo  Speransia wakati  wa mchezo wa kirafiki kati ya  timu ya  watuma  salam mkoa  wa Iringa na  timu ya  watangazaji  wa kituo cha  radio Furaha  Fm ambapo mchezaji Speransia  alipata  kuchezea timu ya  watuma salam na  kuwa binti  pekee katika  timu  hiyo  ya  wanaume  ila aliweza  kuwahenyesha  watangazaji wa radio  Furaha Fm japo  ndio  iliyoweza  kushinda kwa magoli 2-0 dhidi ya  watumasalam

Mwandishi  wa makala  haya ni milimiki wa mtandao  wa www.matukiodaima.com

No comments: