Thursday, January 22, 2015

NAIBU WAZIRI WA UJENZI AKAGUA KIVUKO CHA MV UTETE WILAYANI RUFIJI MKOANI PWANI

Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge(wa kwanza) akishuka ngazi mara baada ya kukagua kivuko cha MV-Utete ambacho hakitoi huduma ya usafirishaji kutokana na kupungua kwa kina cha maji cha mto Rufiji.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA), Eng. Manase Ole-Kujan (wa kwanza kushoto) akitoa taarifa ya kivuko cha MV- Utete kwa naibu waziri wa ujenzi Eng. Gerson Lwenge.
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge (wa pili kulia) akitoa maelekezo na maagizo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA), Eng. Manase Ole-Kujan baada ya kukagua kivuko cha Mv-Utete wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Muonekano wa kivuko cha MV-Utete ambacho kimeegeshwa na kusitisha huduma zake kutokana na kupungua kwa kina cha maji cha mto rufiji.
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge (wa kwanza kulia) akimpa pole Mkuu wa mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo kufuatia mauaji ya askari polisi wawili katika kituo cha polisi cha Ikwiriri Wilayani Rufiji.

No comments: