Monday, August 29, 2016

Mradi wa Kuwezesha Umilikishaji Ardhi ( LTSP ) Wapokelewa na Wananchi Wilayani KILOMBERO

Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga akitoa Mada kuhusu Ujenzi na Ukarabati wa Masjala za Ardhi katika Kijiji cha Sululu Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro,Uhamasishaji huu unaendelea unafanywa pia katika Vijiji Vingine unafanywa na Wizara ya Ardhi, kupitia Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi (LAND TENURE SUPPORT PROGRAME - LTSP),Programu hii inafanya utekelezaji wake ndani ya Miaka mitatu katika Wilaya za Malinyi, Kilombero na Ulanga, Mkoano Morogoro.
Baadhi Wananchi ambao ni Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Sululu wakiangalia ramani ya masjala ya Ardhi, inayotakiwa kujengwa katika kijiji hicho,kupitia Programu ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi,(LAND TENURE SUPPORT PROGRAME - LTSP), mradi ambao upo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mmoja wa Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Sululu Wilayani Kilombero, akichangia Mada iliyowasilishwa na Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga, iliyokuwa ikihamasisha Ujenzi wa Masjala ya kijiji,ambapo pamoja na mambo mengine,itatumika kuhifadhi hatimiliki za kimila (CCROs),ambazo zitatolewa baada ya Programu ya kupima Ardhi za Vijiji katika wilaya za Mfano za Malinyi, Kilombero na Ulanga kukamilika.
Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga katika Meza Kuu akiwa pamoja na watumishi wengine kutoka Wizara ya Ardhi pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Sululu ( kushoto) na Mtendaji Kata kushoto kwake,akiandika kitu kwenye karatasi zake ili kuweka kumbukumbu sawa,wakati wa mkutano wa kuhamasisha Ujenzi wa masjala ya Kijiji,kupitia Programu ya kuwezesha umilikishaji Ardhi (LAND TENURE SUPPORT PROGRAME) - LTSP ),mradi ambao upo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi.
Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga ( watatu kushoto ) waliosimama akiwa kwenye Picha ya Pamoja na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Sululu Wilayani Kilombero, Morogoro.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Sululu, akifungua mkutano wa Kuhamasisha Ujenzi wa Masjala za Ardhi Wilayani Kilombero, Kupitia Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi ( LAND TENURE SUPPORT PROGRAME - LTSP ) mradi ambao unasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga,kupitia Programu ya LTSP chini ya Wizara ya Ardhi inayotekelezwa katika Wilaya za Malinyi, Kilombero na Ulanga Mkoani Morogoro, akitoa Semina elekezi Juu ya Mradi huo, wenye lengo la kupima mipaka ya vijiji na kutoa hatimiliki pamoja na kuhamasisha Ujenzi wa masjala za Ardhi kwenye Vijiji.
Sehemu ya Umati wa Wananchi wa Kijiji cha Sululu Wilayani Kilombero wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Kuongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga,kuhusu umuhimu wa ujenzi wa Masjala ya Kijiji,kupitia Programu ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi(LANDA TENURE SUPPORT PROGRAME),Mradi unaosimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Kaimu kamishna wa Ardhi nchini Bi Mary Makondo, akifafanua Jambo kwa Waandishi wa habari wilayani Ulanga, kuhusu mradi wa Kuwezesha Umilikishaji Ardhi katika Wilaya za Malinyi, Kilombero na Ulanga, ikiwemo upimaji wa Mipaka ya Vijiji na Utoaji wa hatimiliki kwa Vijiji 37 vya Wilaya hizo.
Mratibu wa Mradi wa Kuwezesha Umilikishaji Ardhi, ambao upo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ndugu Godfrey Machabe akizungumza Jambo Mbele ya Kaimu Kamishna wa Ardhi, Bi Mary Makondo muda mfupi Baada ya kumalizika kwa Kikao na Watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kuhusu utekelezwaji wa Mradi wa LTSP.
Picha zote na Hannah Mwandoloma

MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA JWTZ, JKT MGULANI YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM


Meja Dora Kawawa wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa 831 KJ Mgulani (kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula, Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, Dar es Salaam leo jioni , ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambapo kilele chake kitakuwa Septemba Mosi mwaka huu.
Maofisa wa Jeshi wa kikosi hicho wakifurahi na watoto wa kituo hicho baada ya kutoa msaada wao.
Msaada ukitolewa.
Hapa ni furaha pamoja na watoto hao.

Watoto wakipata msaada huo.
Watoto wakipokea msaada.
Hapa ni furaha tupu kwa watoto kwa kupokea msaada kutoka kwa wazazi wao hao.
Picha ya pamoja na watoto hao na viongozi wao.


Na Dotto Mwaibale

JESHI la Kujenga Taifa Kikosi 831 Kj Mgulani limetoa msaada wa vyakula na sabuni kwa watoto waishio Makao ya Taifa ya Watoto Wenye Shida Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo kwa niaba ya mkuu wa kikosi hicho Dar es Salam , Meja Dora Kawawa alisema ni moja ya sehemu ya maadhimisho ya kusherehekea miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

"Tumeamua kushiriki shughuli za kijamii kama kutoa msaada na kufanya usafi ikiwa ni kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa jeshi letu ambapo kilele chake kitakuwa Septemba mosi mwaka huu" alisema Kawawa.

Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance alishuru JKT kwa msaada huo na kueleza ni muhimu sana kwa watoto hao na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kujenga taifa bora la kesho.

Kampuni ya TTCL kusaidia mchezo wa riadha nchini.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (kushoto) akimkabidhi tuzo kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia) iliyotolewa na TTCL kwa mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil hivi karibuni. Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya viongozi wa vyama vya riadha Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (kulia) akimkabidhi tuzo mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL. Wanaoshuhudia katikati ni baadhi ya wanariadha waliyoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (wa kwanza kulia kulia) akimkabidhi tuzo mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL. Wanaoshuhudia katikati ni baadhi ya wanariadha waliyoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo.
Kushoto ni wachezaji wa timu ya Taifa Tanzania walioshiriki katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2016 yaliofanyika hivi karibuni jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil wakirejesha bendera ya taifa kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa tatu kulia) kwenye hafla ya chakula cha jioni kuwapongeza wachezaji iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (katikati) akizungumza kuwapongeza wachezaji hao. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (kulia) wakiwa katika hafla hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi king'amuzi cha DSTV mwanariadha Alphonce Simbu (kushoto) aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil. Kampuni ya TTCL imetoa fedha kwa washiriki wote wa mchezo huo ikiwa ni ishara ya kuwapongeza na kuwatia moyo ili waweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza kwenye hafla ya chakula cha jioni kuwapongeza wachezaji wa timu ya Taifa Tanzania walioshiriki katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2016 yaliofanyika hivi karibuni jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil. Kampuni ya TTCL imetoa fedha kidogo kwa washiriki wote wa mchezo huo ikiwa ni ishara ya kuwapongeza na kuwatia moyo ili waweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo. 
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Antony Mtaka akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliounda timu ta Taifa ya Tanzania kushiriki mashindano ya Olimpiki 2016 Rio. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo kwa mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil hivi karibuni. Tuzo ya TTCL pamoja na zawadi kwa wanariadha walioshiriki mashindfano hayo ilikabidhiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. Kulia ni baadhi ya maofisa wa TTCL wakiwa na tuzo hiyo. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (kushoto) akimkabidhi tuzo kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia) iliyotolewa na TTCL kwa mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil hivi karibuni. Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya viongozi wa vyama vya riadha Tanzania.
Baadhi ya maofisa wawakilishi wa TTCL wakipiga picha ya pamoja na timu ya riadha iliyoiwakilisha Tanzania mashindano ya Olimpiki 2016 Rio, nchini Brazil.

KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) inafanya mazungumzo na vyama vya mchezo wa riadhaa nchini pamoja na wachezaji wa mchezo huo ili kuandaa mpango utakaowawezesha wanaridha kufanya mazoezi ya kutosha na hatimaye kufanya vizuri katika mashindano yao mbalimbali. Kauli hiyo imetolewa jana na Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo alipokuwa akitoa tuzo kwa mmoja wa wanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil hivi karibuni. Mwanariadha Simbu alishika nafasi ya tano katika mbio za marathoni na kuvunja rekodi kwa wanariadha wa Tanzania. 

Kampuni ya TTCL mbali ya kutoa tuzo na fedha zitakazomsaidia mchezaji huyo akiwa mazoezini kwa sasa, imetoa fedha kidogo kwa washiriki wote wa mchezo huo ikiwa ni ishara ya kuwapongeza na kuwatia moyo kutokata tamaa ili waweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano mengine yajayo. "...Kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura TTCL tumejiunga na wadau wengine wa michezo katika kuwapongeza wanamichezo wa timu ya Taifa ya Tanzania walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil, TTCL kwa nafasi yetu tumejiweka mstari wa mbele katika kuwasaidia wanamichezo wa riadha, tumejitolea kufanikisha timu ya riadha katika kukaa vizuri kimichezo..," alisema Mushi. 

"...Katika kipindi hiki cha michezo 2016 tumejitolea kuifanikisha timu ya riadha kuweza kushiriki vizuri katika programu za mazoezi, leo wakati wanarejea tumewaunga mkono kwa kutoa tuzo na fedha kwa msindi aliyefanya vizuri mwaka huu na pia kutoa fedha kwa wanamichezo wetu zitakazo wawezesha kufanya vizuri katika mazoezi yao, huu ni mwanzo lengo letu ni kwamba tutaweka utaratibu mzuri wa kuzungumza na vyama pamoja na taasisi zinazosimamia michezo hii ili kuona tunatengeneza utaratibu mzuri zaidi ambao ni endelevu utakaosaidia kukua kwa mchezo huu," 

alisisitiza meneja uhusiano huyo. Tuzo ya TTCL kwa Alphonce Simbu na fedha kwa wanariadha hao zilikabidhiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambapo aliwapongeza wanamichezo wote wa timu ya tanzania iliyokwenda nchini Brazil kwenye mashindano ya Olimpiki 2016 kwa uzalendo waliouonesha kwa taifa licha ya changamoto anuai. Waziri Nnauye aliwaomba Watanzania kutowakejeli wanamichezo hao kwa maneno ya kuwakatisha tamaa na badala yake kuungana kuwapongeza na pia kutoa ushauri kwa wadau wa michezo ili Tanzania iweze kufanya vizuri katika mashindano yajayo, ikiwa ni pamoja na vyama vya michezo kusaidia kyuongeza idadi ya wachezaji wa timu ya Tanzania. 


Kampuni ya Multichoice Tanzania pia iliungana na TTCL na kuwazawadia ving'amuzi vya DSTV vilivyolipiwa kwa muda wa miezi sita wanamichezo wote wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya Olimpiki mwaka 2016, pamoja na kumsaidia kumuwezesha mwanariadhaa Simbu programu za mazoezi kwa muda wa mwaka mmoja akiwa kama balozi wa kampuni hiyo. Timu ya Taifa ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya Olimpiki mwaka 2016 ilikuwa na wanamichezo saba, ambapo wanamichezo wanne walishiriki riadha, wawili waogeleaji na mmoja alishiriki mchezo wa judo.

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AKIWA KWENYE ZIARA NAIROBI.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais na Ofisa mtendaji Mkuu wa kampuni ya Sumitomo Corporation ya Japan, Bw. Kunihuru Nakamura  katika Mkutano wa TICAD 6 uliofanyika Nairobi Kenya, Agosti 28, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais na Ofisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sumimoto Corporation ya Japan katika mkutano wa TICAD 6 uliofanyika jijini Nairobi Agosti 28,2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Sumimoto ya Japan, Bw. Kanihuru Nakamura  (kushoto kwake) baada ya mazungumzo yao jijini Nairobi Agosti 28, 2016. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Profesa James Mdoe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt.Adelhelm Meru.  Wanne kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia  Masuala ya Wakimbizi, Fillipo Grand kabla ya mazungumzo yao jijini Nairobi, Agosti  28, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE, Bw. Edwin Rutageruka (kushoto) wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016. 
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Wananchi wa Kanda ya Ziwa zaidi ya 750 wapata mafunzo Kilimo Biashara jijini Mwanza.

Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama akitoa salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa kongamano hilo (hawapo pichani).

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumzia malengo ya Kongamano la Kilimo Biashara kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) kufungua rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akitoa hotuba ya kufungua Kongamano la Kilimo Biashara kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk. Charles Mahika akielezea mikakati iliyowekwa na wizara ya kuhakikisha sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo inafanikiwa.
Mwezeshaji ambaye pia ni Rais wa vijana wajasiriamali na wataalamu wa miradi ya maendeleo mkoa wa Singida, Philemon Kiemi akitoa mafunzo ya ufugaji kuku wa kisasa kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
Mratibu wa Kongamano kutoka ESRF, Abdallah Hassan akizungumza jambo kwenye kongamano hilo.
 Mwezeshaji Bi. Kalega akitoa mafunzo ya ufugaji Kuku na matumizi ya Azolla kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
Baadi ya wakazi wa Kanda ya Ziwa akiwemo mke wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bi. Mongella waliohudhuria Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.

Na Mwandishi wetu
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, limesema litaendela kuinua fursa za kiuchumi zinazopatikana hapa nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa zinazoendelea kuibuliwa.

Kauli hiyo imetolewa na Programme Specilist- Inclusive Growth UNDP Tanzania, Ernest Salla wakati wa Kongamano la Kilimo Biashara kanda ya ziwa lilofanyika katika ukumbi wa Rocky City Mall Agosti 27 mwaka huu Jijini Mwanza.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii  (ESRF) kwa kushirikiana na UNDP/UNEP lililolenga kuzitambulisha fursa katika kilimo biashara, lilihudhuriwa na wananchi mbalimbali zaidi ya 750 kutoka mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza wenyewe.
Katika kongamano hilo Salla alisema kilimo kina fursa nyingi hivyo watanzania hawana budi kuzitumia fursa hizo kwa kuwakumbatia wataalamu ili kiwe mkombozi wa maisha yao.

Akizungumza katika Kongamano hilo la siku moja, Mkurugenzi wa ESRF Dk Tausi Kida alisema licha ya uchumi wa taifa kutegemea kwa kiasi kikubwa kilimo, lakini kilimo hapa nchini bado kipo nyuma  hivyo kuchangia kiasi kidogo katika kumuendeleza mkulima.

“Kwa kutambua upungufu huu, ESRF ikishirkiana na UNDP/UNEP imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali ili kusaidia wananchi na taifa kwa ujumla kujikwamua katika vizingiti mbalimbali vya maendeleo ukiwemo umasikini wa kipato,” alisema Dk Kida

Alisema kukua kwa teknolojia duniani, kumeongeza fursa nyigi za kimaendeleo ikiwamo kilimo, kwani wakulima wengi hivi sasa hawategemei mvua na hutumia eneo dogo kwa ajili ya kilimo.

Katika warsha hiyo zilitolewa mada mbalimbali; pamoja na kilimo cha Foda (Hydroponic fodder), kilimo cha mbogamboga (Hydroponic and Aquaponic Vegetables), shamba kitalu (Green house), Azolla na  ufugaji wa samaki na nyuki kutoka kwa wakufunzi mbalimbali waliotoa ufafanuzi kuhusu fursa mpya za kilimo biashara.

Alisema kilimo cha kisasa au “smart farming” ambacho hakihitaji maeneo makubwa kinaweza kufanyika katika maeneo ya mjini tofauti na izaniwavyo kuwa kilimo lazima kiwe vijijini.

Alisema ESRF imeshiriki katika utekelezaji wa miradi ya majaribio inayotegemea teknolojia ya kisasa katika wilaya  za Bunda, Bukoba vijijini, Sengerema, Nyasa, Ikungi na Ileje kupitia miradi ya PEI na CDRBM kwa kipindi cha miaka mitatu.
Pamoja na mambo mengine, alisema matokeo ya miradi hiyo ya majaribio yamethibitisha fursa katika kilimo biashara yanayoweza kuwasadia wananchi katika kujikwamua na ndio miongoni mwa sababu ya kuandaa warsha hiyo.

Akifungua kongamno hilo ambaye alikuwa mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella alisema kilimo pekee ndicho chenye fursa pekee rahisi kuliko sekta nyingine duniani kote.

Mongela aliipongeza ESRF, UNDP, na wadau wengine wa maendeleo, kwa  tafiti hizo na kwamba hatua hiyo itasaidia kuinua uchumi wa watanzania na taifa kwa ujumla.

 Licha ya Mongella kupongeza hatua hizo, lakini alizitaka taasisi mbalimbali kupitia wataalamu wake kuonyesha gharama halisi za kutekeleza miradi hiyo.

“Hizi tekonolojia ni rahisi, watu wakianza nazo kidogokidogo baadaye watapanda na kufika juu, tatizo la wataalamu wanasema gharama ni kubwa za teknolojia, hivyo kuwaogopesha watu,” alisema Mongella

Amoni Manyama kutoka UNDP, alisema kuzingatia maelekezo ya wataaalamu ndio njia pekee ya kufanikisha katika kubuni fursa za kilimo na biashara.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk Charles Mahika alisema wizara yake ikishirikiana nan chi zinazozunguka Ziwa Victoria wanaandaa mwongozo wa kuanzisha ufugaji wa samaki katika vizimba na kwamba mwongozo huo unatarajiwa kukamilishwa jijini Mwanza hivi karibuni.

Katika kongamano hilo wapo baadhi ya wananchi waliotoa shuhuda mbalimbali walionza kunufaika na fursa za kilimo biashara chini ya ufadhili wa UNDP ikishirikiana na ESRF.